Na mwandishi wetu, Dodoma
KATIBU Mkuu Ofisi ya Rais Utumishi, Bw. Juma Mkomi, ameupongeza Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kwa kushiriki na kutoa huduma katika Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma kwenye viwanja vya Chinangali jijini Dodoma Juni 22, 2026.
“Niwapongeze sana kwa ushiriki wenu, lakini pia kwa kutoa elimu na kuhudumia wananchi, naamini katika maonesho haya mmekutana na wanachama wenu wengi, hongereni sana,” alisema Bw. Mkomi.
“Hadi kufikia leo alasiri Juni 22, 2026, jumla ya wananchi 365 walitembelea kwenye banda letu, na tumewahudumia vizuri, wengi wao wameunganishwa na huduma za kidijitali (PSSSF Portal),” alisema Meneja Rasilimaliwatu PSSSF Bi. Gloria Mboya wakati akitoa maelezo kwa Katibu Mkuu Mkomi.
Kwa kutumia simu janja au kompyuta wanachama anaweza kuongia kwenye PSSSF Portal kuangalia michango yake, kuwasilisha madai mbalimbali na kufatilia, kuhuwisha taarifa zake na za wategemezi wake, na kwa wastaafu wanaweza kujihakiki.
Maonesho ya Wiki ya Utumishi wa Umma yaliyobeba kaulimbiu isemayo ‘Kuchochea Uwajibikaji Jumuishi kwa Huduma Endelevu’ yanatarajiwa kufikia kilele Juni 23, 2026.

More Stories
Wananchi wapata elimu ubora,usalama na bidhaa
Matumizi magari ya umeme kuongeza umuhimu gesi asilia
Serikali yataka ulinzi,uwezeshaji wajane