Na mwandishi wetu,Timesmajira
Mkutano wa kilele cha wiki ya uhuru wa kiuchumi 2026 na uzinduzi wa taarifa ya u tafiti wa ukaguzi Leo umekamilika kwa wajumbe kutoa mapendekezo ambao umeangazia mambo mbalimbali.
Akizungumza jijini kwenye uzinduzi wa ripoti maalumu Mkurugenzi wa Taasisi ya Library SParks Denis Exaud amesema kuwa muhimu ya majadiiano sera, tafiti na mapendekezo yatakayosaidia kuinua mazingira ya biashara na uwekezaji nchini.
Nitumie fursa hii kutoa pongezi za dhati kwa Dkt. Samia suluhu Hassani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Uongozi wake thabiti na wenye maono katika Kuimarisha uchumi wa Taifa kupitia sera za mageuzi ya kiuchumi, Diplomasia ya kimkakati ya uchumi na uwekezaji mkubwa katika miundombinu

Aidha ameeleza kuwa uzinduzi huu unaoyesha taarifa ya ukaguzi wa uhuru wa kiuchumi nchini na uwepo wa ishara ya dhamira ya serikali ya kuendelea kusikiliza ajenda ya mageuzi ya kiuchumi nchini,
Mkuu huyo ameeleza kwamba katika mchakato wa utafiti wadau waliwasilisha mapendekezo muhimu yanayohusu uthabiti wa sera shindani wa kikodi, mageuzi ya kidijitali , biashara za kimataifa, ulinzi wa mikataba,ubunifu wa teleolojia, maendeleo ya ujenzi wa nguvu kazi, mageuzi ya serikali za mitaa pamoja na haki ya kumiliki Mali.

More Stories
Silinde azindua baraza la sita la Wafanyakazi Tume ya Taifa ya Umwagiliaji
NMB ilivyosaidia Serikali kukusanya zaidi ya Sh trilioni 9.8
Serikali yaongeza nguvu kwa wachimbaji wadogo,yasisitiza usalama Migodini