March 16, 2026

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

FIFA na TFF yaanza utambuzi wa vipaji vya Watoto mkoani Rukwa

Na Israel Mwaisaka, Rukwa


Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF kwa kushirikiana na shirikisho la kimataifa la mpira wa miguu (FIFA) limeanza utambuzi wa vipaji vya watoto wenye umri chini ya miaka kuanzia 12-16 mkoani Rukwa ambao watashindanishwa kuanzia ngazi ya wilaya kisha kuingizwa kwenye timu ya Taifa ya vijana.

Hayo yamebainishwa na mkuu wa Idara ya utambuzi wa vipaji kutoka shirikisho la Mpira wa miguu TFF Gidion Ngereza wakati wa utambuzi wa vipaji vya vijana katika Halmashauri nne (4) za mkoa wa Rukwa na kubainisha kuwa lengo ni kutafuta vipaji vya Watoto wenye umri kuanzia miaka 12-16 ambao wataingizwa kwenye timu ya Taifa ya vijana na kwamba zoezi hilo linafanyika katika mikoa 32 na Halmashauri 184 nchini Tanzania.

Aidha ametoa wito kwa wazazi na walezi kuendelea kuwaruhusu Watoto wao kushiriki kwenye mashindano hayo kwani yatawawezesha kupata Watoto bora na mahili ambao mwisho wa siku watakuwa na uwezo wa kujiri kupitia sekta ya Michezo.

Hata hivyo zaidi ya Watoto 180 mkoani Rukwa wamechaguliwa ili kushindanishwa kwenye michezo hiyo kwa ngazi ya mkoa kati ya hao 11 wakitokea Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi.