
Na Mwandishi Wetu, Mlele.
Watu watatu wa familia moja wamefariki dunia kufuatia ajali ya moto baada ya nyumba waliyokuwa wakiishi kuteketea kwa moto katika Kijiji cha Ilunde, Wilaya ya Mlele mkoani Katavi.
Mmoja wa ndugu wa familia hiyo, Wiliam Maganga, amesema tukio hilo lilitokea usiku wa kuamkia Machi 6, 2026, ambapo moto huo ulisababishwa na mlipuko wa mafuta ya petroli yaliyokuwa yamehifadhiwa ndani ya nyumba, baada ya familia hiyo kusahau kuzima jiko la mkaa.

Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.
Akizungumzia tukio hilo baada ya kushiriki shughuli za maziko kijijini hapo, Mkuu wa Wilaya ya Mlele, Majid Mwanga, amewataka wananchi kuepuka kuhifadhi mafuta ya petroli ndani ya nyumba kwa kuwa ni hatari.
Amesema waliofariki ni mama wa familia Holo Sheka (32) pamoja na watoto wake wawili, Peter Paschal (6) na Tabitha Paschal (3). Baba wa familia na watoto wengine watatu wamejeruhiwa na wanaendelea kupatiwa matibabu katika Kituo cha Afya Ilunde.


More Stories
Wanawake waaswa kuwaelimisha mabinti kujiingiza katika shughuli za kiuchumi
Wahariri waipongeza REA usambazaji wa Gesi Asilia Lindi,Pwani
Dkt.Kimaro:Hakuna serikali inayoweza kuwaajili wahitimu wote wanaomaliza Shule