Na Mwandishi Wetu, Timesmajira Online, Mwanza
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mwanza imemuachia huru aliyekuwa, Mkuu wa Mkoa wa Simiyu,Dkt.Yahaya Nawanda baada ya kupokea na kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili na kutomkuta na hatia.
Dkt.Nawanda,alishitakiwa kwa kumuingilia kinyume na maumbile mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustine(SAUT),kampasi ya Mwanza(jina limehifadhiwa),kosa linalodaiwa alitenda Juni 2,2024,kinyume na kifungu cha 154,kifungu kidogo cha 1,cha kanuni ya makosa ya adhabu sura ya 16.Ambapo mshitakiwa huyo kwa mara ya kwanza alipandishwa kizimbani katika Mahakama hiyo Julai 9, mwaka huu.
Ambapo Dkt Nawanda,ameshindwa kutiwa hatiani katika kesi ya Jamhuri namba 1883 ya mwaka 2024, baada ya Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo,Erick Marley,kusema kuwa ushahidi katika kesi hiyo,umekuwa ukikizana,hivyo kutia shaka kama mshitakiwa huyo alitenda kosa hilo kama lilivyopelekwa mbele yake.
Akitoa hukumu Novemba 29,2024,baada ya kesi hiyo kusikilizwa kwa miezi minne,Hakimu huyo amesema ushahidi uliotolewa na upande wa Jamuhuri umeacha shaka katika maeneo mbalimbali ikiwa ni pamoja na video mjongeo ‘CCTV footage’, zilizowasilishwa kutokuonesha sehemu wawili hao walikuwa kwenye gari wakitenda tukio hilo.
Huku sehemu nyingine ilioacha shaka ni mlalamikaji(mwanafunzi huyo),kutokwenda hospitali kwa wakati na ushahidi unasema alienda baada ya saa 19 baada ya tukio.Pia kutowasilishwa kwa kielelezo cha kisayansi(DNA), chenye kuthibitisha kama mshitakiwa ndiye aliyetenda kosa hilo au lah.
Pia sehemu nyingine ya ushahidi kukizana ni mlalamikaji alidai kufanyiwa kitendo hicho ndani ya gari nyeupe yenye vioo vya giza(tinted),tofauti na ushahidi wa vielelezo vilivyowasilishwa Mahakamani hapo likiwemo gari lenye rangi ya fedha lenye vioo vyeupe isiyo na tinted.
Kwa upande wake Dkt.Nawanda,amemshukuru Mungu,familia yake na Mahakama kwa kutenda haki.
More Stories
CPA.Makalla:Wananchi ondoeni dhana ya CCM kushinda kwa kubebwa
CCM yataka ushirikiano kwa viongozi waliochaguliwa kwenye uchaguzi serikali za mitaa
Wadau wa jinsia wataka NAOT kufanya ukaguzi unaozingatia jicho la jinsia