April 23, 2024

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bingwa wa kuunga mifupa kwa miti shamba – Tabibu Makingili

Na David John, timesmajira online

MAKAM wa Rais wa shirika la Madawa Asili Tanzania Tameto Islam Makingili ambaye pia ni mtafiti wa dawa za asili na mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha waganga wa Tiba Asili Tanzania Shivyatiata amewataka watanzania kukitumia kituo cha Islam Herbal Medicin Center kilichopo Makambako Mkoani Njombe ili kutibu Maradhi yanayowasumbua ikiwa Pamoja na maradhi ya kuvinjika mifupa wanaunga na mgonjwa anarudi katika hali yake ya awali.

Makingili ameyasema haya leo Julai 31 mwaka huu mkoani humo wakati akizungumza na waandishi wa habari katika Ofisini za kituo hicho zilizopo katika mji wa Halmashuri ya Makambako Mtaa wa Posta, ambapo amesema kuwa watanzania wengi wanakabiliwa na maradhi mbalimbali kwenye miili yao hivyo kupitia kituo hicho wanatibu maradhi hayo.

Mkurugenzi wa kituo cha Islam Herbal Medicine Center Tabibu Islam Makingili akizungumza na waandishi wa Habari ofisni kwake Halmashauri ya Mji wa Makambako mkoani Njombe, juu ya umuhimu wa tiba Asili julai 31, 2022

Amesema kuwa Islam Herbal Medicin Center inaunga mifupa kwa wale wanaovunjika pia wanatibu magonjwa sugu yaliyoshindikana hata katika hospitali za kawaida kama vile kaswende,Gono,Uti,vidonda vya tumbo na hata kansa huku akiwataka wagonjwa hao kwenda na vipimo ambavyo wamepima katika hospitali kwa lengo la kujiridhisha kabla ya kuwapatia huduma.

“kwa kifupi nimeaza shughuli hizi tangu miaka ya 1973 nikiwa kijana mdogo hadi sasa hivyo nina uhakika na kile ambacho ninakifanya na katika kipindi hicho chote sijawahi kukutana na changamoto zozote zaidi ya kuokoa maisha ya watu kutokana na maradhi wanayokabiliana nayo.”amesema Makingili

Tabibu Islam Makingili akionyesha chumba Maalum cha kuungia mifupa.kwenye kituo chake. julai 31, 2022

Pia ameongeza kuwa pamoja na mambo mengine lakini pia ni mtafiti nakwamba ili uwe mganga mzuri lazima ufanye tafiti za kutosha hivyo katika hilo amejiridhisha kwa asilimia mia moja juu ya dawa ambazo anawatibia watu na kwa bahati nzuri wagonjwa wenyewe wanaleta shuhuda baada ya kupona.

Akizungumzia zaidi kuhusu huduma hiyo Makingili amesema licha ya uwepo na kituo hicho mkoani Njombe lakini pia anakituo kama kingine mkoani Ruvuma katika wilaya ya Songea mjini ambapo pia wanaunga mifupa na kutoa huduma zingine kutokana na maradhi mbalimbali yanayowasumbua binadamu.

Tabibu Islam Makingili akionyesha sehemu Maalumu ya kuhifadhi dawa. julai 31, 2022

Aidha amefafanua kuwa licha ya kutibu kaswende ,Gono,Vidonda vya Tumbo,Kansa pia anatibu kizazi kwa wanawake anazibua mishipa na kuimarisha mishipa hiyo kwa upande wa wanaume na hiyo ni kutokana na kukabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwamo msongo wa mawazo (stress) kipato, nakadhalika.

Tabibu Makingili ambaye anapatikana kwa mawasiliano ya 0768337248 au 0715542028 amesema kupitia kituo chake watu wengi wamepona na huku akiishukuru Serikali kupitia Ofisi ya Mganga mkuu wa mkoa huo kwa ushirikiano anao upata .

Tabibu Islam Makingili akionyesha chumba maalum cha mganga katika kituo hicho cha Islam Herbal Medicine center. julai 31, 2022

“Hapa nataka niseme kuwa Mafanikio yote ambayo yapatikana yanatokana na kufanya kazi kwa kufuata utaratibu na sheria zinazotuongoza kwa mfano mimi hapa nina usajili na ninafanya kazi zangu kwa kufuata misingi ya vibari niliovyonavyo.”amesema Tabibu Makingili

Nakuongeza kuwa “hapa mimi kama kuna mgonjwa ambaye hali yake hairidhishi basi nawasiliana na ofisi ya mganga mkuu na wanakuja kumchukua ili kuweza kumpatia huduma zingine na kimatibabu na hata wale wanaoshindikana hospitalini wanakuja kwangu hapa wakiwa na vyeti vyao na wanapona bila wasiwasi.hivyo na wakaribisha.”amesisitiza Tabibu Makingili