May 27, 2022

Timesmajira

Gazeti Huru La Kila Siku

Bado jamii ina mwamko mdogo matumizi miti shamba,vyakula asili

Na Mwandishi Wetu,TimesMajira, online,Dar

IMEELEZWA kuwa jamii bado ina mwamko mdogo juu ya matumizi miti shamba na vyakula asili hii ni kwa sababu ya kukosa elimu ya kutosha juu ya Matumizi hayo huku wanaume wakionekana kuwa na elimu zaidi .

Hayo yamebainishwa Jijini Dar es Salaam na Ofisa Mazingira kutoka Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na utoaji elimu kuhusiana na masuala mbalimbali likiwemo suala la Utunzaji wa Mazingira (Envirocare) Euphrasia Shayo wakati akizindua wiki ya kijani ambayo imeanza kufanyika Oktoba 7 hadi 31,mwaka huu, ambapo nchi 52 zinashirikiana lengo zaidi likiwa kutoa elimu kwa jamii uu ya utunzaji wa mazingira na kujali afya za binadamu chini ya ufadhili wa Shirika lisilo la kiserikali la Swedish Society for Nature Conservation.

Amesema uelewa matumizi ya miti shamba na vyakula vya asili bado ni mdogo kutokana jamii kuchukuliwa kawaida zaidi masuala hayo.

“Chagamoto bado ni elimu ikitolewa itasaidia kwa kiasi kikubwa kuezi vyakula vya asili pamoja na miti dawa kwa ajili ya utunzaji wa mazingira pamoja na kwa afya ya binadamu”amesema na kuongeza kuwa

“Wakati tunafanya utafiti tuligundua kuwa watu wenye elimu zaidi juu ya miti shamba ni wanaume kuliko wanawake hii ni kutokana na tamaduni zilizopo mwanaume ndio uenda kutafuta dawa mashambani”ameongeza

Akitolea mfano amesema katika kipindi cha janga UVIKO 19 jamii ilijikita katika kutumia vyakula vya asili pamoja na kuimiza kutumia dawa aina ya miti shamba .

“Watu wengi walikuwa wakitumia dawa mbadala kama vile tagawizi pamoja na viungo mbalimbali lengo hasa likiwa kuimarisha afya na kujenga kinga ya mwili”amesema .

Amesema Envirocare imeandaa wiki ya kijani ili kutoa elimu kwa jamii kuhusu masuala mazima ya mazingira ambapo mwaka huu imejikita hasa katika madawa ya asili na vyakula vya asili.

Shayo amesema Envirocare imejipanga kufanya utafiti wa kugalia aina mbalimbali za dawa katika mkoa wa Tanga wilaya Muheza ambapo aina mbalimbali ya madawa ya asili ambayo yameweza kutumika kwa muda mrefu sambamba na kuangalia madawa hayo yanaitwaje, upatikaniji wake pamoja na matumizi yake.

“Tutatoa elimu hii kwa kuhakikisha kwamba jamii nzima ya mijini na vijijini inapata uelewa wa kutosha juu ya masuala mbalimbali yanayohusu miti shamba pamoja na vyakula vya asili”amesema.

Amebainisha kuwa shirika hilo lilianza Shughuli hizo za utafiti mwaka 2020 na kuona kwamba elimu hiyo bado aijaweza kusambaa katika maeneo mengi hasa mijini .

Ofisa Mazingira kutoka Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na utoaji elimu kuhusiana na masuala mbalimbali likiwemo suala la Utunzaji wa Mazingira (Envirocare ) Euphrasia Shayo akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kuzindua
wiki ya kijani ambayo imeanza kufanyika Oktoba 7 hadi 31,mwaka huu ambayo itashirikiana na nchi 52.

Amesema Shirika hilo litaendelea kutoa elimu endelevu katika jamii kama njia ya kuhakikisha vizazi vijavyo vinakuwa na uelewa wa kutosha juu miti shamba pamoja na vyakula vya asili katika maisha ya kila siku.

Shayo alifafanua kuwa katika utafiti uliofanyika mwaka jana waliweza kugundua kuna miti dawa mingi ambayo imekuwa ikipatikana Tanzania huku wazawa katika maeneo hayo wakionekana kuitumia na kujua umuhimu wake.

Amesema mwaka huu shirika hilo limeanzisha bustani maalumu ambayo itaoteshwa miti dawa aina mbalimbali zaidi ya 52

“Lengo la bustani hii ni kutumika kama eneo la kujifunzia ambapo mwaka jana tulipata wanafunzi 102 ambao walikuja katika bustani hiyo na kujifunzia juu ya miti mbalimbali ambayo imeoteshwa ikiwemi kujua matumizi yake ya kutibu maradhi mbalimbali”amesema

Amesema katika utekelezaji wa mradi huo watafanya kazi kwa kushirikiana na mtaalamu ambaye ni Mwanabailojia amekuwa akifahamu zaidi juu ya miti hiyo na namna ya kuitumia.